AFISA Elimu awali na Msingi Saada Chwaya na timu yake wamefanya ufuatiliaji wa Shule tatu Magingo,Mkongotema,na Lipupuma Kata ya Mkongotema Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.
Mara baada ya Ufuatiliaji huo Chwaya ameongea na walimu kwa awamu tofati juu ya uboreshaji wa utunzaji wa mazingira na kutunza miundo mbinu ya Shule, kufundisha wanafunzi nidhamu pamoja na kuhakikisha wanafunzi wa awali,lakwanza na darasa la tatu wanamudu kusoma,kuandika na kuhesabu.
Hata hivyo Afisa Elimu ametoa rai kwa walimu hao kuhakikisha wanafunzi wote kuanzia darasa la awali hadi darasa la saba wawe wanakula shuleni.
Afisa Elimu akigawa chakula kwa Wanafunzi katika Shule mpya ya Msingi Lipupuma.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Februari 28,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa