• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

HALMASHAURI ya Madaba yaingiza milioni 191 kutokana na mauzo ya Mazao Mnadani

Posted on: November 16th, 2020

HALMASHAURI ya Wilaya ya Madaba imeingiza zaidi ya shilingi milioni 191 ya mauzo ya mazao mnadani katika msimu wa mwaka 2019/2020.

Akitoa taarifa hiyo ofisini kwake  Afisa Kilimo,Umwagiliaji na  Ushirika (W) wa Halmashauri hiyo Joseph Mrimi ameyataja Mazao ya yaliyouzwa kupitia vyama vya ushirika kuwa ni Korosho na Kahawa, Ufuta na Soya.

Mrimi amevitaja vyama vya Mazao vilivyojiunga na vyama vikuu vya ushirika MBIFACU,SONAMCU,TAMCU ikiwa kimoja kimejiunga na SONAMCU na vyama vitano TAMCU vyama viwili.

“Utaratibu wa mauzo unafanyika kwa mfumo wa stakabadhi  ya mazao ghalani  ambapo vyama vinakusanya mazao ya wakulima na kupeleka mnadani na mazao hayo yakiuzwa kunakuwa na makato ya kisheria”,alisema.

 Afisa Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika huyo amesema kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani wakulima wanapata changamoto kama upungufu wa maghala yenye sifa,ukosefu wa Elimu ya juu ya mfumo wa stakabadhi ghalani na kuchelewesha malipo ya wakulima.

 Mrimi  ameongeza kuwa AMCOS ni vyama vya msingi vya ushirika wa mazao na SACCOS ni vyama vya ushirika  vya akiba na mikopo na ametoa rai kwa wananchi kujiunga na vyama hivyo ili waweze kunufaika.

Kwa mujibu wa Mrimi, Halmashauri ya Wilaya ya Madaba ina jumla ya vyama vya ushirika nane, vyama vya ushirika vya mazao(AMCOS),vitano ambavyo  ni Wino (AMCOS, TAMA,AMCOS,MbangamaweAMCOS,Madaba AMCOS, (Mbonane AMCOS) na vyama vya kuweka na kukopa (SACCOS)  vitatu ambavyo ni Wino SACCOS,Muungano Gumbiro SACCO na Mahanje SACCOS.

Hata hivyo amesema Kuna baadhi ya SACCOS hazifanyi vizuri kutokana na uongozi wa SACCOS kutokuwa waaminifu,na ukosefu wa elimu ya juu na maswala ya fedha kwa watendaji wa SACCOS.

Mrimi amesema wananchi wa Madaba wananufaika na SACCOS kwa kujiwekea akiba  na fursa ya kupata mikopo yenye  masharti nafuu kwa ajili ya kuendesha shughuli zao kupitia SACCOS.

Imeandaliwa na Aneth Ndonde

Afisa Habari Halmashauri ya Madaba

Novemba 16,2020.

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • UJENZI WA MADARASA 2 NA MATUNDU 6 YA VYOO SHULE YA MSINGI KIPINGO WAKAMILIKA KWA ASILIMIA 100

    May 30, 2025
  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Chwaya atoa rai kwa walimu wa awali kutekeleza agizo la Serikali

    January 18, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa