HALMASHAURI ya Wilaya ya Madaba wamefanya kikao cha tathimini ya utekelezaji wa afua za Lishe kwa kipindi cha robo ya tatu Januari hadi Machi 2023.
Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Madaba na Mgeni rasmi katika kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Songea Wilman Ndile.
Afisa Lishe wa Halmashauri hiyo Neema Bernadi akitoasoma taarifa amesema mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha robo tatu ikiwemo kufanya tathimini ya hali ya Lishe kwa Wanafunzi 39 wa clabu ya Lishe ya Shule ya Sekondari Madaba na kuwapa unasihi.
Hata hivyo Afisa Lishe huyo ameeleza changamoto zilizojitokeza kwa kipindi cha miezi mitatu pamoja na wazazi wengi msimu wa kilimo wanatumia muda mwingi kwenye shughuli za kilimo kuliko kuzingatia malezi na matunzo ya watoto na wajawazito na kuathiri hali ya Lishe.
“Kuto kujengewa uwezo wa masuala ya lishe kwa waratibu wa Lishe ngazi ya vituo vya huduma ya afya kupelekea kuathiri utoaji wa huduma sahihi za lishe’.
Hata hivyo amesema mikakati ya kuwafikia wananchi pamoja na kuendelea kufanya maadhimisho ya siku ya Afya na Lishe ya Kijiji ili kuwezesha Elimu ya Lishe kuwafikia watu wengi zaidi,kuimarisha utoaji wa Elimu kupitia wahudumu wa Afya na jamii.
“Halmashauri itaendelea kuunda clab za Lishe na kuhamasisha utekelezaji wa Shughuli za Lishe ikiwemo uanzishwaji wa bustani za mboga mboga na matunda”.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Mei 9,2023
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa