HIFADHI ya Misitu Wino Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Mkoa wa Ruvuma inajumla ya hekta 39,718 zilizoundwa kwa safu tatu Ifinga,Mkongotema na Wino.
Akisoma taarifa hiyo Meneja wa Shamba la Miti Wino Grory Fotunatus katika kikao cha wadau wa misitu kilichofanyika leo Novemba 10,2023 katika ukumbi wa Amani Madaba.
Amesema hekta 13,140 zimehifadhiwa kwaajili ya vyanzo vya maji ,misitu ya asili na mabondeni kwaajili ya wanyama na viumbe hai wengingi.
Fotunatus amesema msitu huo umeanza kuendelezwa mwaka 2010 ukihusisha eneo dogo safu ya Wino na mwaka 2014 walienedeleza safu ya Ifinga na Mkongotema.
Hata hivyo Muhifadhi Mkuu amesema wameendelea kuongeza eneo la upandaji miti kila mwaka hekta 400 hadi 500,ufugaji wa nyuki,misitu na mazingira yote ya asili na vyanzo vya maji ili kuhakikisha uhifadhi unakuwa endelevu kwa kizazi cha sasa na baadae.
“Kwa kuanzisha maliasili na vyanzo vya maji vinatunzwa kama mto lupahila,mnywamasi,mwesa,Lutukila,Mgombezi,Kineneka,kipilili,balali mapacha,chechengu,mito inayofikisha maji yake ziwa nyasa na mto Rufiji”.
Amesema uhifadhi huo unasaidia kuongeza ajira za kudumu na mkataba kila mwaka ikiwa eneo la upandaji linaongezeka na mazao ya biashara kama nguzo za umeme, ufugaji wa nyuki ili kuongeza mapato ya Serikali.
“Tunaboresha mazingira na madhari ukipita ndani ya hifadhi utapata hali nzuri ya hewa na kupunguza hewa okaa na kuvutia mazingira ikiwa kuanzia Mwaka 2010 hadi 2023 imepandwa hetka 6463 ya miti”.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Novemba 15,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa