MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amepokea taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Akizungumza katika kikao kazi hicho kilichohudhuriwa na Wakuu wa Wilaya ,Kamati ya ulinzi ya usalama,pamoja na viongozi wa Taasisi mbalimbali ya Mkoa amesema lengo ni kujua miradi inayotekelezwa mkoani hapo ilipofikia.
“Nimepokea taarifa kutoka idara mbalimbali naomba viongozi kuwa wamoja na kujadili changamoto zilizopo na kuzitatua kwasababu wote tunajenga nyumba moja”.
Ibuge amewaagiza wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha wanasimamia miradi yote,ikiwemo vituo vya afya kutoa huduma bora pamoja na miradi ya Elimu inayojengwa kumalikika kwa wakati.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Afisa Habari Halmashauri ya Madaba
Mei 27,2021
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa