• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

JUKWAA la kuboresha uhifadhi wa ushoroba wa Selous Niassa Lafunguliwa Ruvuma

Posted on: December 11th, 2020

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amefungua Jukwaa la kuimarisha uhifadhi ushoroba wa Selous Niassa ambalo limefanyika kwa siku mbili  kwenye ukumbi wa Heritage Cottage mjini Songea.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Jukwaa hilo Mndeme amewaagiza wadau wa uhifadhi mkoani Ruvuma kuhakikisha kuwa ushoroba wa wanyamapori wa Selous Niassa unaimarika na kufikia malengo ya kunufaisha jamii za kizazi cha sasa na kijacho.

“Eneo la ushoroba wa Selous Niassa limebarikiwa kuwa na utajiri mkubwa wa rasilimali mbalimbali za mimea,wanyamapori,ndiyo maana Pori la Akiba la Selous limechaguliwa na UNESCO kuwa urithi wa dunia na kuanzishwa kwa Hifadhi ya Taifa ya Nyerere’’,alisema Mndeme.

Amesema ushoroba huo una makundi makubwa ya wanyamapori kama tembo,mbwamwitu,nyati,viboko na simba na kwamba ushoroba huo ni muhimu kwa hifadhi mbili za Tanzania na Msumbiji yaani Selous na Niassa.

Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa Mkoa,sekta ya utalii nchini inaingiza pesa nyingi za kigeni kwa kuwa inaleta wageni milioni 1.5 kwa mwaka na kwamba utalii pekee unachangia pato la Taifa kwa asilimia 17 na kutoa ajira kwa watanzania milioni mbili.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Uwanda wa Ruvuma wa Shirika la WWF Diana Shuma amesema jukwaa hilo la Mkoa ni la pili kufanyika likihusisha ushoroba wa Selous Niassa na kwamba kikao hicho kinawakutanisha wadau ili kujadili namna ya kuhifadhi ushoroba huo ambao upo katika hatari ya kutoweka.

Amesema ushoroba huo ni muhimu kwa Tanzania na Msumbiji kwa kuwa ni mapitio muhimu ya wanyamapori na unakabiliwa na changamto ya watu kufanya shughuli za kiuchumi ikiwemo kilimo na ufugaji.

“Lengo la kuanzisha jukwaa hili ni kuwaleta pamoja wadau  kujadili na kutengeneza mikakati ya kuhifadhi ushoroba huu wa Selous Niassa ambao una ukubwa wa hekta zaidi ya milioni  1.5’’,alisisitiza Shuma.

Fidel Kimario ni Mratibu Uhifadhi Wanyamapori na mapito ya wanyama Wizara ya Maliasili na Utalii amesema serikali imeandaa kanuni za kusimamia mapito ya wanyamapori ili kukabiliana na hatari ya kutoweka mapito ya wanyamapori.

Enock Msocha ni Kaimu Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Kanda ya Kusini Mashariki wa TAWA inayohusisha mikoa ya Lindi,Mtwara na Ruvuma,amesema wameongeza mbinu mbalimbali za kulilinda pori la Selous ikiwemo kuongeza doria katika maeneo yote wakati wote.

Hata hivyo amesema wanashirikiana na wananchi katika maeneo jirani ya hifadhi kufanya ulinzi na kufuatilia wanyama kwa karibu endapo wamevuka katika maeneo ya wananchi ili wananchi na wanyama waweze kuwa salama.

Imendikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Desemba 11,2020

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Chwaya atoa rai kwa walimu wa awali kutekeleza agizo la Serikali

    January 18, 2025
  • MARATIBU wa mradi wa BOOST Madaba amshukuru Rais Samia

    January 18, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa