MAADHIMISHO ya siku ya wanawake Duniani mwaka 2022 yawakumbusha kutokomeza visababishi vya umaskini katika ngazi ya Kaya na kunyimwa haki katika umiliki wa rasilimali ardhi.
Akizungumza Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akiwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo amewapongeza Wanawake na amewashukuru kwa kumpa fursa ya mwaliko wa sherehe hizo.
Ibuge amesema kwa kuzingatia kauli mbiu ya siku ya wanawake Duniani mwaka 2022 Kizazi cha Haki na usawa kwa Maendeleo Endelevu; Tujitokeze Kuhesabiwa inatukumbusha kama jamii na Taifa kuweka mipango sawia inayozingatia kizazi cha Haki na Usawa.
Amesema tunapokumbushana kupitia sherehe hizi tunaadhimia kuhakikisha kwamba tunaendeleza jitihada za pamoja kama Taifa ,kama Mkoa, kama Jamii kwamba mila na desturi ambazo zinakinzana na ulinzi wa Haki za Mwanamke tunazitokomeza na zile ambazo zinatufaa kwa uhimilivu wa jamii zetu tunazienzi.
‘’Serikali ya awamu ya siata imesimamia kidete katika kulinda haki na kujenga usawa kwa jamii ikiwemo kumiliki ardhi, kumpiga mwanamke, ubakaji, kutelekeza mwanamke na familia”.
Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Ruvuma Xzavelia Mlimira amesema siku hii ya wanawake inatumika kama siku rasmi ya kuikumbusha dunia juu ya haki za wanawake na kuongeza chachu katika harakati za mapambano katika usawa wa kijinsia.
Akisoma Risala Mwakilishi wa wanawake Mariamu Juma amesema maadhimisho haya yanakumbusha na kuelimisha jamii juu ya haki za binadamu hususani wanawake na watoto.
Hata hivyo ameongeza kuwa maadhimisho ya mwaka huu yamejikita katika kauli mbiu inayotusaidia kutambua kuwa wanawake na wanaume tunajukumu la pamoja la kuleta maendeleo kwenye jamii kwa kushiriki katika maeneo mbalimbali yakiwepo ya kimaamuzi kuanzia ngazi za kifamilia hadi Taifa.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Ofisi ya Habari ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Machi 9 2022.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa