Timu ya wataalam Halmashauri ya Wilaya ya Madaba imefanya ziara ya kutembelea miradi ya Maendeleo kwa lengo la kujionea thamani ya miradi inayotekelezwa.
Miradi hiyo ni pamoja na utekelezaji wa ujenzi wa Kituo cha afya Matetereka kilichojengwa kwa shilingi milioni 562 kwa mradi wa tozo mwaka 2021/2022 Milioni 500 ililetwa kwa awamu mbili na mapato ya ndani mwaka 2022/2023 Halmashauri ilitoa milioni 42 mwaka 2023/2024 Halmashauri ilitoa Milioni 20.
Hata hivyo ujenzi huo unahusisha majengo manne OPD,mama na mtoto, maabara na jengo la kufulia pamoja na kichomea taka majengo hayo yamefikia hatua ya ukamilishaji na kuanza kutoa huduma.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Machi 5,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa