Idara ya Maendeleo ya Jamii ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba kwa kushirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kutoka Shamba la Miti Wino, wamefanya matendo ya huruma katika Vituo vya Afya vya Mtyangimbole na Madaba leo Machi 03, 2026. Matendo hayo yamelenga kuwafariji na kuwasaidia wagonjwa pamoja na wahudumu wa afya kama sehemu ya kuonesha mshikamano wa kijamii.
Hatua hiyo ni sehemu ya maandalizi kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, yanayoadhimishwa kila mwaka tarehe 08 Machi, ambayo yanatoa fursa ya kutambua mchango wa wanawake katika jamii.
Kimkoa, maadhimisho yatafanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea, huku kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba yakitarajiwa kufanyika siku ya Ijumaa tarehe 06 Machi, 2026. Shughuli zitaanza kwa Bonanza la Michezo litakalofanyika katika Shule ya Msingi Madaba.
Maadhimisho hayo yatahitimishwa kwa hafla ya “Usiku wa Mwanamke” itakayofanyika katika Ukumbi wa Amani, ambapo wananchi wanatarajiwa kushiriki kwa wingi kuonesha mshikamano na kuthamini nafasi ya mwanamke katika maendeleo ya jamii.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa