HALMASHAURI ya Wilaya ya Madaba wamefanya kikao cha kujadili mpango mkakati waTaifa wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA).
Afisa Utawi wa Jamii Shani kambuga ameeleza mwongozo ulioandaliwa kwaajili ya kufanikisha utekelezaji wa mpango kazi wa Taifa wa kutokomeza Ukatili dhidi ya wanawake na watoto ulioanzishwa mwaka wa fedha 2017/2018 na utekelezaji mwaka 2021/2022 hadi 2026.
“Mwongozo unaelekezwa namna ya kuunda kamati na mgawanyo wa majukumu na utendaji wa kamati za ulinzi wa wanawake na watoto kuanzia ngazi ya Taifa ,Tawala za Mikoa hadi Mamkala za Serikali za Mitaa”.
Amesema kamati hiyo imefanikiwa kutoa elimu kwa jamii juu ya ukatili wa wanawake na watoto katika shule za msingi 20 na shule 6 za sekondari na mikutano ya hadhara vijiji na mitaa.
“Halmashauri kupitia idara ya afya ,ustawi wa jamii na lishe,maendeleo ya jamii na dawati la jinsia Wilaya imeendelea kutoa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa jamii kwa kushirikiana na vyombo vya sheria katika kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto,vipigo,unyanyasaji,ndoa za utotoni kwa jamii”.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Julai 26,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa