HALMASHAURI ya Wilaya ya Madaba imevuka lengo la utoaji wa chanjo ya Surua na Rubella jumla ya watoto 8010 sawa na asilimia 115.
Akizungumza katika kikao cha tathimini ya utekelezaji wa kampeni ya chanjo ya surua na Rubella kwa watoto wenye umri kuanzia miezi 9 hadi 59 mratibu wa chanjo mwenzeshaji wa chanjo Alex Magasha amesema surua na Rubella yanasababishwa na Virusi vya morbillvirus vinavyoenea kwa haraka na kuathiri watu wa lika zote hasa watoto wenye umri chini ya miaka mitano.
Magasha amesema magonjwa haya kuenea kwa njia ya hewa hususani mgonjwa anapokohoa au kupiga chafya na maambukizi kuenea kwa haraka sehemu zenye msongamano.
Hata hivyo amesema ugonjwa wa Surua na Rubella unadalili kama vile homa,kutokwa na upele vidogo vodogo ambavyo huanza usoni,nyuma ya masikio na kusambaa mwili mzima,mafua na kikohozi na macho kuwa mekundu na kutoa machozi.
“Madhara ya ugonjwa wa Surua na Rubella masikio kutoa usaha na kusababisha kuto sikia,Nimoni,Utapia mlo,vidonda vya macho vinavyoweza kusababisha ulemavu wa kuto kuona,ulemavu kwa mtoto na kupoteza maisha”.
Amesema utekelezaji wa wa kampeni katika halmashauri ya Wilaya ya Madaba ilitekeleza zoezi la utoaji wa chanjo ya Surua na Rubella katika vituo 21 ambavyo vinatoa huduma za chanjo.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Agosti 28,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa