• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

MAHAFARI Ya Kidato cha Nne Magingo yafana Madaba

Posted on: September 28th, 2023

SHULE ya Sekondari Magingo Kata ya Mkongotema Halmashauri ya Madaba wamefanya Mahafari ya 12 kwa wanafunzi wa kidato cha nne 2023.

Mgeni rasmi katika Mahafari hayo amekuwa Mbunge wa Jimbo la Madaba Joseph Mhagama amewakilishwa na Mwenyekiti wa Halamshauri ya Madaba Teofanes Mlelwa amewapongeza Walimu kwa kuhakikisha wanafunzi hao wanahitimu Elimu ya Kidato cha nne na kuwazawadia Sukari kilo 25 itakayowasaidia kupata chai Shuleni hapo.

“Mimi nimewapa zawadi Walimu kwasababu natambua mchango   wenu mzuri kwa wanafunzi hawa kwa kuishi nao hapa shuleni miaka mine na kuwapa Elimu ambayo itawasaidia kuingi kidato cha tano”.

Mkuu wa Shule hiyo Said Kunemka akisoma taarifa kwa Mgeni ramsi amesema Shule hiyo ilianzishwa rasmi mwaka mwaka 2009  na kusajiliwa rasmi kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo namba S .3979 na kupewa namba ya kituo cha mtihani S.4086 na Baraza la Mitihani.

Kunemka amesema Shule hiyo inajumla ya wanafunzi 292 ikiwemo wavulana 112 na wasichana 180  na inawalimu 16 wakiume 8 na wakike 8 pamoja na watumishi wasio walimu 7.

Hata hivyo amesema mafanikio ya ufaulu wa kidato cha nne wa shule hiyo kwa mda wa mika mitatu mfululizo Mwaka 2020 walifanya mtihani wanafunzi 31 na waliofaulu walikuwa 29,Mwaka 2021 walifanya mtihani wanafunzi 35 na walifaulu wanafunzi 32 pamoja na mwaka 2022 walifanya Mtihani wanafunzi  53 walifaulu 44.

“Mafanikio yanayotekelezwa kupitia Serikali ya awamu ya sita Shule hiyo imefikiwa na huduma ya Maji salama na wanafunzi kujipatia maji ya kutosha na kupata mda wa kujisomea,huduma ya umeme,huduma ya miundombinu kama vile maabara ,uwepo wa walimu wa kutosha,upatikanaji wa mashine ya kukoboa na kusaga”.

Amesema upatikanaji wa Televisheni ya Shule iliyonunuliwa na Mbunge wa Jimbo la Madaba Joseph Kizito Mhagama pia ameishukuru Serikari inayoongozwa na Rais Samia.

Imeandaliwa na Aneth Ndonde

Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba

Septemba 28,2023.

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Chwaya atoa rai kwa walimu wa awali kutekeleza agizo la Serikali

    January 18, 2025
  • MARATIBU wa mradi wa BOOST Madaba amshukuru Rais Samia

    January 18, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa