MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Chritina Mndeme amepongeza Mkoa wa Ruvuma hali mavuno ya mazao ya chakula kwa mwaka 2019/2021 kwa kuvuna tani 1,355,509 na Mkoa kuchukua nafasi ya kwanza kitaifa.
Akitoa taarifa hiyo katika kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa jana amesema mahitaji ya chakula katika Mkoa ni tani 469,172 ziada ni tani 886.337 Mkoa umeendelea kufanya vizuri katika uzalishaji wa mazao ya Kilimo kwa mara ya pili mfululizo.
“Mafanikia haya ni matokeo ya wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kwa kuendelea kujituma katika shughuli za kilimo bila kulazimishwa na usimamizi mzuri wa maafisa ugani Ugani na viongozi wa Serikali”.
Mdeme amesema mazao ya Ufuta,Mbaazi,na Soya kwa mwaka huu katika Mkoa wetu umefanyika kupitia mfumo wa stakabadhi ya Mazao ghalani na kusaidia kupatikana zaidi ya shilingi bilioni 28.
Akitoa mchanganuo huo amesema Mapato ya Ufuta ni zaidi ya shilingi bilioni 25,Soya zaidi ya shilingi bilioni moja na Mbaazi zaidi ya shilingi bilioni bili.
Amesema Mkoa unaendelea kushirikiana na Taasisi zingine za Serikali katika kusimamia zoezi la ununuzi wa Korosho kutoka kwa wakulima hadi sasa imeuzwa kilo 14,826,644 zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 33.
Hata hivyo Mndeme amesema msimu wa Kilimo wa Mwaka 2020/2021 umelenga kulima hekta 672,137 za mazao ya chakula ,Bustani na kutarajia kuvuna tani 1,790,582,amesema mafanikio katika kilimo yanatokana na matumizi bora ya pembejeo za Kilimo.
Mndeme amesema Serikali katika msimu wa mwaka 2020/2021 itaendelea na mfumo wa bei elekezi wa kununua pembejeo za kilimo hususani Mbolea ya kupandia (DAP) na ya kukuzia (UREA),na Wizara ya Kilimo pamoja na mamlaka ya udhibiti wa ubora wa Mbolea Tanzania(TFTA)imetoa bei elekezi kwa kila Wilaya.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Afisa habari Halmashauri ya Madaba
Januari 13,2021
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa