• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

MWENYEKITI wa Halmashauri Madaba atoa rai kwa Madiwani kusimamia mradi wa Boost

Posted on: May 19th, 2023

MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Teofanes Mlelwa amewasisitiza Waheshimiwa Madiwani Kusimamia Miradi ya Boost.

Hayo ameyasema katika  kikao cha Baraza la Madiwani cha robo  ya tatu ya  mwaka 2022/2023.

Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Halmashauri Mwenyekiti amesema Waheshimiwa Madiwani wasimamie miradi ya  Boost  inayojumuisha ujenzi wa Madarasa ya Shule za Msingi na Awali na kuhakikisha inakamilika kwa wakati.

Afisa Elimu Vifaa na takwimu msingi  Raphael Kibiligi ambaye ni mratibu wa Mradi huo amempongeza Rais Samia kwa kuleta  fedha Milioni 610,300,000/= kwaajili ya ujenzi wa shule mpya ya Lipupuma  na madarasa maalumu ya awali katika Shule ya Msingi Ifugwa pamoja na vyoo 6.

Hata hivyo Kibiligi amesema pia fedha hizo za mradi wa Boost zitatumika katika ujenzi wa madarasa 8 katika shule nne tofauti.

“Sisi kama Halmashauri tumejipanga kuhakikisha tunatekeleza mradi huu kwa wakati na kumaliza kwa wakati na kujenga majengo ambayo yataendana na thamani ya fedha ambayo tumepata”.

Kibiligi amesema mpaka kufikia sasa wametoa Elimu kwa jamii pamoja na kutamburisha  mradi huo na baadhi ya maeneo wameshaanza kutekeleza mradi ikiwemo shule ya Lipupuma wameshaasafisha eneo la ujenzi.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Matumbi  Valentino Mtemauti ametoa shukrani za dhati kwa Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia,kwa  kutoa fedha nyingi kwaajili ya mradi wa Boost unaowezesha uboreshaji wa shule za msingi na awali.

Hivyo Mtemauti  amewaomba Madiwani ambao fedha zimeenda katika Kata zao kuhakikisha wanasimamaia kwa weledi ili Halmashauri iendelee kuletewa fedha kwaajili ya miradi mingine ya Maendeleo..

Imeandailiwa na Aneth Ndonde

Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

Mei 19,2023

 

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Chwaya atoa rai kwa walimu wa awali kutekeleza agizo la Serikali

    January 18, 2025
  • MARATIBU wa mradi wa BOOST Madaba amshukuru Rais Samia

    January 18, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa