• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

Nchimbi alivyompongeza Mbunge wa Jimbo la Madaba

Posted on: April 19th, 2024

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Imanuel Nchimbi amewapongeza wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kwa kumpokea kwa shangwe na ndelemo   mara baada ya kuwasili katika Mkoa huo Jimbo la Madaba akitokea Mkoa wa Njombe.

Nchimbi akizungumza na Wananchi ametoa salamu kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa ushirikiano na amempongeza Mbunge wa Jimbo la Madaba kwa niaba ya chama cha mapinduzi kwa kutoa ardhi itumike kwaajili ya Chama cha mapinduzi.

“Kwa uungwana ulionao Mbunge umekabidhi viwanja na majengo yaliyopo tunakushukuru sana”.

Hata hivyo Nchimbi amesema Mbunge wa Jimbo la Madaba kwa kutambua watendaji waliopo kwenye Jimbo lake ametoa pikipiki 8 katika kata kwa makatibu  wa chama na baiskeli 45 kwa makatibu wa matawi.

“Nikisema CCM haitamani kuwa na Wabunge wa namna hii nitakuwa muongo inapenda kuwa na wananchama na viongozi ambao wapo tayari kujitoa na kujitolea kwaajili ya chama na Nchi”.

Hata hivyo amesema alichokifanya Joseph Mhagama  siku ya leo amenikumbusha historia ya viongozi wakati wa kupigania Uhuru walitoa mali na  fedha zao kwaajili ya TANU,ikiwa watu maskini kabisa walichangia shilingi moja ili Mwalimu Nyerere aweze kwenda kupigania uhuru katika umoja wa Mataifa New York.

Nchimbi amesema kwa kuwa wananchi wa Jimbo la Madaba ni wachapakazi na wakulima wakubwa hivyo atahakikisha chama cha mapinduzi kitaendelea kusimamia Serikali kuwa pembejeo za kilimo zinapatikana kwa wakati.

Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

Aprili 19,2024. 

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Chwaya atoa rai kwa walimu wa awali kutekeleza agizo la Serikali

    January 18, 2025
  • MARATIBU wa mradi wa BOOST Madaba amshukuru Rais Samia

    January 18, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa