Halmashauri ya Wilaya ya Madaba imepokea fedha kiasi cha shilingi milioni 314. kutoka Serikali Kuu kupitia mradi wa BOOST kwa mwaka wa fedha 2025/2026 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya katika Kata ya Lituta, Halmashauri ya Madaba mkoani Ruvuma.
Ujenzi huo utahusisha miundombinu ya elimu ya awali na msingi, ukiwa na lengo la kuboresha upatikanaji wa elimu kwa watoto wa kijiji cha Lituta na maeneo ya jirani.
Kupatikana kwa fedha hizo ni sehemu ya juhudi endelevu za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika kusogeza huduma muhimu kwa wananchi na kuimarisha miundombinu ya elimu nchini, ili kuhakikisha kila mtoto anapata haki ya msingi ya elimu bora.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa