MRADI wa SEQUIP umewanifaisha wanafunzi walioacha masomo kutokana na sababu mbalimbali kuazia miaka 13 hadi 21.
Akizungumza Afisa Elimu ya watu wazima Sekondari Halmashauri ya Madaba Edward Wellah alipowatembelea wanafunzi hao katika Shule ya Madaba Sekondari,Mahanje na Wino ametoa rai kwa walimu kuwafundisha kama watu wazima bila kujua changamoto zao zilizowafanya wanafunzi hao kuacha masomo yao hapo awali.
“Naomba muwafundishe kama watu wazima bila kuwachapa viboko,kuwafanyisha usafi hata kuwakaripia kwa namna moja au nyingine”
Wellah amewaomba wanafunzi hao kuhudhuria masomo yao kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa saba kamili mchana na kutokata tamaa ikiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Watanzania ameona mbali katika swala nzima la kuwapa kipaumbe watoto wa kike kusoma bure kupitia mradi huo.
Amesema mradi huo katika Halmashauri ya Madaba utakuwa katika Shule sita za Sekondari ikiwemo Madaba day,Ifinga,Mahanje,Wino,Ngumbiro na Nguluma.
Kwa upande wake Mkufunzi John Mapunda amesema mradi huo utakuwa na hatua mbili ya kwanza watasoma kidato cha kwanza na cha pili na kufanya Mitihani ya Taifa hatua ya pili watasoma kidato cha tatu na cha nne na kufanya mtihani wa Taifa ya kidato cha nne.
Hata hivyo Mkufunzi amesema faida za mradi huo kwa wanafunzi ambao watafaulu kuingia hatua ya pili Serikali itawalipia Bima ya Afya na wataendelezwa kusomeshwa.
“Mjitahidi kusoma hata kama mnaona mda ni mchache mmepata fursa ukiona unachangamoto waoneni walimu na walimu muwasaidie hawa wanafunzi waweze kufikia malengo yao”.
Amesema RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameona kwa jicho la tatu ili kuhakikisha watoto wa kike ambao waliacha masomo yao wanarudi shuleni na kuhakikisha Serikali inawagharamia ada ili waweze kutimiza malengo yao .
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Februari 20,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa