MKOA wa Ruvuma umeingia mikataba 13 na wakandarasi ambayo ni yahatua ya pili sawa na asilimia 40 yenye jumla ya zaidi ya shilingi bilioni 6.
Mkuu wa Ruvuma Kanal Laban Tomas akizungumza katika hafla hiyo amesema mikataba hiyo iliyosainiwa ni utekelezaji wa hatua ya pili kwa mwaka fedha 2022/2023.
Amesema mikataba hiyo inahusisha mikataba mitano ya jimbo itakayogharimu zaidi ya jumla ya kiasi cha shilingi bilioni 2 ikiwemo mikataba sita ya tozo itagharimu zaidi ya shilingi bilioni 2,mkataba mmoja wa matengenezo kupitia mfuko wa barabara utakaogharimu kiasi cha fedha zaidi ya shilingi milioni 200 na mkataba wa fedha maalumu kutoka serikali kuuutagharimu kiasi cha fedha zaidi ya shilingi milioni 700.
Hata hivyo amesema Utekelezaji wa mikataba hiyo unaanza mwezi Oktoba na kumalizika mwezi Februari 2022 na kumalizika 2023 hivyo Mkuu wa Mkoa ametoa rai walioisaini mikataba kuhakikisha wanazingatia mda wa kuanza na kukamilisha pamoja na kuzingatia ubora wa kazi.
“Serikali haitasita kumchukuliahatua mkandarasi yeyote atakayekwenda kinyume na makubaliano yaliyomo katika mkataba”.
Mkuu wa Mkoa ametoa rai kwa Wakala wa Barabara za vijijini na mjini Mkoa wa Ruvuma kuhakikisha wanasimamia kazi kwa uadilifu mkubwa ili malengo yanayokusudiwa yakalimike.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Octoba 21,2022.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa