Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mh Rais *Dkt. Samia S. Hassan* imetenga fedha katika bajeti ya mwaka 2023/24 kwa ajili ya utekelezaji mkubwa wa miradi ya umwagiliaji katika bonde la Mto Ruvuma,Ruhuhu na Litumbandyosi yaliyopo mkoani Ruvuma.
Hayo yamesemwa jana na Naibu Waziri wa Kilimo *Mh. Anthony Mavunde* wakati wa ziara ya Makamu wa Rais *Mh.Dkt. Philip Isdor Mpango* katika Wilaya za Nyasa na Mbinga,Mkoani Ruvuma.
Akizungumza na wananchi wa wilaya za Mbinga na Nyasa,Makamu wa Rais Dkt. Mpango aliwapongeza wakulima wa Mkoa wa Ruvuma kwa mchango wao mkubwa kwenye usalama wa chakula hapa nchini kutokana na uzalishaji mkubwa wa mazao ya nafaka hasa mahindi na kutumia fursa hiyo kuitaka Wizara ya Kilimo ieleze jinsi ilivyojipanga katika utekelezaji wa miradi ya umwagiliaji.
Akitoa maelezo ya Wizara ya Kilimo Naibu Waziri Mavunde Mavunde amesema Serikali itaendelea kusimamia utekelezaji wa miradi mikubwa ya umwagiliaji mkoani Ruvuma ili kuongeza uzalishaji wa mazao.
-Kwa mwaka wa fedha 2023/24 Serikali itafanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina na ujenzi wa miumbombinu ya Umwagiliaji katika Bonde la Mto Ruvuma lenye jumla ya hekta *26,066*,Mto Ruhuhu lenye hekta *3,700* na Litumbandyosi hekta *900* pamoja na uchimbaji wa mabwawa makubwa matano(5) na ukarabati wa skimu za umwagiliaji katika wilaya mbalimbali za Mkoa wa Ruvuma.
Amesema wakulima Mkoa wa Ruvuma wamezalisha zaidi ya tani milioni 1 ya mahindi,ni mkoa ambao serikali itawekeza kiasi kikubwa kwenye kilimo cha umwagiliaji ili kuongeza uzalishaji wa mazao.
-Serikali itaendelea kusimamia upatikanaji wa soko la uhakika la mazao ya wakulima,na kwasasa Wakala wa Hifadhi ya Chakula(*NFRA*) wamefungua vituo *17* vya ununuzi wa Mahindi katika wilaya za Mkoa wa Ruvuma.
-Mbolea za Ruzuku zitaendelea kutolewa kama msimu uliopita,na kwasasa tumesajili vituo vingi zaidi vya mauzo ya mbolea ili wakulima wasiifute mbolea umbali mrefu kama ilivyokuwa msimu uliopita.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa