• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

TAKUKURU Ruvuma imejipanga kuchunguza hoja za Mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali

Posted on: August 2nd, 2021

TAASISI ya kupambana na rushwa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma wamejipanga kufanya uchunguzi Katika Halmashauri zote katika Upotevu wa fedha zaidi ya bilioni 3 katika mfumo wa mashine za Pos.

Akitoa taarifa hiyo Mkuu wa TAKUKURU Mkoa  wa Ruvuma Hamza Mwenda amesema wameendelea kutekeleza majukumu yake katika robo ya nne ya mwaka wa fedha 2020/2021 iliyoanzia Aprili hadi Juni 2021.

“Vipaumbele vya kipindi cha mwezi Julai hadi Septemba kufanya uchunguzi wa hoja ya Mdhibiti na mkaguzi  wa Hesabu za Serikali katika ubadhilifu wa fedha katika  Halmashauri kupitia utaratibu wa POS”

Mwenda amesema katika kipindi hicho cha mienzi mitatu wamefuatilia matumizi ya fedha za umma katika utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo (PETS)na kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa viwango kinachotakiwa na thamani ya fedha inapatikana kwa kuzuia mianya ya rushwa na upotevu wa rasilimali katika Utekelezaji.

Hata hivyo amesema katika hatua nyingine TAKUKURU  Mkoa wa Ruvuma imefanikiwa kufanya ufuatiliaji wa Miradi 5 ya maendeleo yenye thamani ya zaidi bilioni 1 na mapungufu yaliyobainika yametolewa mapendekezo na maboresho kwa mamlaka husika na yameanza kufanyiwa kazi.

TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma katika kipindi cha miezi mitatu wamepokea  taarifa 110 kutoka kwa wananchi kupitia vyanzo mbalimbali na malalamiko yote yalifanyiwa kazi  taarifa 39 zilikuwa za rushwa na taarifa 71 hazikuhusu rushwa  hivyo watoa taarifa walishauliwa namna bora ya kutatua kero zao.

“TAKUKURU inayotembea tumeweza kusikiliza kero za wananchi katika maeneo mbalimbali na kutatua kero hizo katika kijiji cha Ndongosi  Halmashauri ya Wilaya ya Songea na Maweso Halmashauri ya Mdaba”.

Mwenda amesema wamepokea malalamiko 8 yalihusu ubadhilifu katika vyama vya msingi vya ushirika –AMCOS,Migogoroya ardhi,ubadhilifu wa fedha kupitia force account,matatizo ya mirathi na viongozi wa vijiji kutooa taarifa za mapato na matumizi ya fedha za vijiji.

Mwenda amesema wamejipanga kuongeza uelimishaji Umma kwa kutumia njia mbalimbali kushiriki katika maonesho ,mbio za mwenge matamasha ya uelimishaji,semina kwa watendaji pamoja na kufanya chambuzi za mifumo katika maeneo yanayolalamikiwa zaidi kama maeneo ya utoaji wa huduma katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo sekta ya Elimu,Ununuzi,Kilimo na Afya.

Imeandaliwa na Aneth Ndonde

Afisa Habari Halmashauri ya Mdaba

30,Julai 2021

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Chwaya atoa rai kwa walimu wa awali kutekeleza agizo la Serikali

    January 18, 2025
  • MARATIBU wa mradi wa BOOST Madaba amshukuru Rais Samia

    January 18, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa