Afisa Elimu awali na msingi Saada chwaya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba amewapongeza walimu na kutoa zawadi mbalimbali kwa kuwaheshimisha viongozi wa Halmashauri kwa kuwa wakwanza Kimkoa mtihani wa darasa la saba na darasa la nne 2023.
Pongezi hizo amezitoa katika kikao cha tathimini kilichoambatana na sherehe za kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri.
“Nilijisikia faraja sana katika kikao cha maafisa elimu wa Halmashauri 184 wa Nchi nzima na mikoa 26 Halmashauri 68 tulifikia wastani wa asilimia 85 katibu mkuu wa TAMISEMI alitupatia zawadi ya cheti nikiwemo mimi nawashukuru sana kwa kunihesshimisha walimu wangu”.
Aidha chwaya amewapongeza walimu wanaojitole nao wamekuwa chachu ya kusababisha ufaulu mzuri wa wanafunzi katika Halmashauri.
“Kwa wale walimu ambao hawajapata ajira wameshiriki kutuletea mafanikio mbingu ziwe wazi Mungu apokee dua ajira zinazokuja waajiliwe”.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Mei 17,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa