WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhemishiwa Seleman Jafo anatarajia kuanza ziara ya kikazi mkoan i Ruvuma kuanzia Desemba 16 mwaka huu.Kulingana na ratiba ya ziara hiyo iliyotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Jafo anaanza ziara katika wilaya ya Tundurui ambapo Desemba 16 atakagua ukarabati wa shule ya sekondari Tunduru na mchana ataanza safari ya kuelekea wilaya ya Namtumbo ambako atakagua Kituo cha Afya Mtakanini.
Kwa mujibu wa ratoiba ya ziara hiyo,Waziri Jafo siku ya Desemba 17 atakuwa katika Manispaa ya Songea ambako anatarajia kukagua ujenzi wa barabara za Manispaa ya Songea,ukagua ujenzi wa Machinjio ya kisasa katika Kata ya Tanga na kuhitimisha kukagua kituo kikuu cha mabasi cha Mkoa wa Ruvuma kilichojengwa Kata ya Tanga Manispaa ya Songea
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa