MKURUGENZI Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Sajidu Idrisa Mohamed ametembelea eneo la ujenzi wa madarasa 8 na jengo la utawala utakaogharimu shilingi milioni 331,600,000/= za mradi wa Boost.
Shule hiyo inayojengwa Kata ya Mkongotema shule ya Lipupuma kupitia mradi wa uboreshaji wa Miundombinu ya Shule za Msingi na awali ili kuimarisha upatikanaji wa fursa katika ujifunzaji bora Tanzania Bara (BOOST)
Mkurugenzi amemwagiza Mtendaji Kata kuhakikisha sheria zinafuatwa pamoja na kanuni na taratibu za mradi.
“Hakikisheni mafundi wanapewa mikataba,Ujenzi uanze kwa wakati na kukamilika kwa wakati,majengo yajengwe yenye ubora ili tukikamilisha tupewe fedha zingine”.
Mohamed amempongeza Mh.Diwani wa Kata hiyo Vastus Mfikwa kwa kutoa ushirikiano kuanzia kazi ilipoanza ya kusafisha eneo amekuwa eneo la mradi.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Mei 23,2023
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa