• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Muundo wa Utawala
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika

ZAO la Mkonge linaongoza kwa Soko Duniani

Posted on: January 27th, 2022

MAAFISA ugani wa Mkoa wa Ruvuma wamepewa mafunzo juu ya kanuni bora za kilimo cha Mkonge .

Mafuzo hayo yametolewa na wataalamu kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania [TARI] Tanga katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa Ruvuma.

Mkuu wa mafunzo kutoka Taasisi ya Utafiti ya Kilimo Tanzania Frank Mabagala ameeleza umuhimu wa  Mkonge  kwa sasa kutokana na mabadiliko makubwa ya tabia ya nchi.

 Amesema wakulima wamekua wakikosa mavuno kwa sababu hii TARI kwa kushirikiana na Bodi ya Mkonge Tanzania imeazimia kuhamasisha kilimo cha  Mkonge kwa wakulima wadogo katika maeneo mbalimbali Tanzania ili zao litumike kwa kuwaleta tija kwa wananchi wa Tanzania.

Mtafiti Dietram Mkapa ameeleza umuhimu wa kilimo cha zao la Mkonge halina msimu maalumu wa kupanda na linapokuwa tayari kuvunwa kwa mwaka mara mbili ,hivyo ni zao ambalo linaweza kumpatia mkulima kipato cha uhakika katika kipindi chote cha mwaka.

Mkapa amesema Mkonge ni zao linalostahimili magonjwa na halidhuriwi kirahisi na magugu na majanga mengine kama moto,Pia ameongeza kuwa pembejeo kama mbolea,viuagugu na viuatilifu katika mazingira ya kawaida sio lazima kutumika ingawa matumizi yake yanaongeza uzalishaji wa mavuno ya mapema

Amesema zao la Mkonge linaweza kuchanganywa na mazao mengine kama kunde,maharage,mahindi,alizeti,njegere na karanga.

Mtafiti ameeleza matumizi ya Mkonge kuwa unaweza kutumika katika tasnia ya kilimo,nishati,ujenzi,famasia,magari,meli,majumbani,ofisini na mazingira mengine.

Mkapa amesema   zao la Mkonge soko lake ni la uhakika hupatikana nje ya nchi na ndani ya Nchi mmea wa Mkonge unaweza kuishi kwa kipindi cha miaka 10-25,hivyo kumuhakikishia mkulima kipato cha uhakika na kwa muda mrefu.

”Tubadili kilimo cha Mkonge kutoka uzio kuwa shamba la mkulima mdogo wa Mkonge, Halmahauri itumie zao la Mkonge kama zao mbadala katika maeneo makame na maeneo mengine yaliotelekezwa Pamoja na kutoa mafunzo kwa wakulima juu ya singa na ubora wa singa ,Halmashauri kwa kushirikiiana na Bodi ianzishe vitalu mbegu bora za Mkonge katika maeneo makame”. amesema Mkapa.

 Mkonge ni moja kati ya  zao la biashara Tanzania,Asili ya zao hili ni Mexico na baadae likasambaa katika nchi za India na Tanzania mwaka 1892, Zao la Mkonge liliingizwa nchini na mtaalamu wa kijerumani Dr.Richard Hindorff Ambaye alikua mtafiti wa mimea na udongo,Kutokana na mabadiliko ya hali ya uchumi nchini Tanzania serikali ya Tanzania ilipitisha sheria ya sekta ya mkonge ,1997;ambayo iliruhusu ubinafsishaji wa viwanda vinavyomilikiwa na serikali na kuanzisha Bodi ya Mkonge Tanzania.

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • TANGAZO LA AJIRA ZA SENSA May 05, 2022
  • TANGAZO LA KAZI May 10, 2021
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • MAAFISA Ugani 34 Ruvuma wapatiwa mafunzo ya upimaji wa afya ya udongo

    May 20, 2022
  • MKOA wa Ruvuma watoa chanjo ya polio kwa asilimia 122

    May 20, 2022
  • HALMASHAURI ya Madaba yaazimia kukamilisha miradi kabla ya mwaka wa fedha 2021-2022 kuisha

    May 19, 2022
  • IBUGE azitaka Halmashauri kutoa Mikopo ya asilimia 10 kwa Vikundi vya TASAF

    May 15, 2022
  • Angalia zote

Video

RUVUMA HAINA SHULE YA LITEPATILE,TAARIFA ZILIZOTOLEWA NI UZUSHI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: P.O.BOX 10

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: info@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa