Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Ruvuma ikiongozwa na Mwenyekiti wake Komred Odo Mwisho imekabidhi vitanda 20 vyenye uwezo wa kulaza wanafunzi 40 katika sekondari ya Ifinga Kata ya Matumbi Halmashauri ya Madaba Wilayani Songea vilivyotolewa na Mwekezaji sekta ya Misitu katika kijiji cha Ifinga Sekondari ya Ifinga ina wanafunzi 80 wanaosoma kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne kati yao wavulana 42 na wasichana 38.
Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Ruvuma ikiongozwa na Mwenyekiti wake Komred Odo Mwisho imeendelea na ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Madaba Wilayani Songea.Moja ya miradi ambayo imekaguliwa na Kamati hiyo ni Mradi wa ujenzi wa sekondari mpya ya Lilondo kata ya Wino ambapo serikali imetoa shilingi milioni 560 kutekeleza mradi huo
Wananchi wa kijiji cha Ifinga kata ya Matumbi Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma wamemshukuru serikali kwa kuboresha barabara ya Ifinga yenye urefu wa kilometa 48 kutoka barabara kuu ya Songea-Njombe ambapo hivi Sasa wanatumika saa moja badala ya saa 16.Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ifinga Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Ruvuma Komred Odo Mwisho amesema serikali inatekeleza miradi mbalimbali katika kijiji hicho ikiwemo Uboreshaji wa barabara,miundombinu ya shule ya Msingi,sekondari na afya Kata ya Matumbi ina kijiji kimoja kinachoitwa Ifinga hata hivyo serikali inatekeleza miradi mbalimbali kama ilivyo katika kata nyingine zenye vijiji vingi.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: P.O.BOX 10
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: info@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa